Jimbo la Dimani

Mombasa – Fumba Chaleni · maili 10 mraba · Bahari ya Hindi

Historia ya Elimu

Skuli ya Kombeni maalumu 1980–1992. Tangu 1993 poromoko la elimu.

Wazawa wameamua

Kwa nia moja kuunda JUMEDI – kupambana na changamoto za kielimu

JUMEDI imara

Ili kuwajengea uwezo vijana, kupunguza umaskini, kujenga utawala bora

Utangulizi: Jimbo la Dimani

JUMEDI – Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Jimbo la Dimani. Ni jumuiya isiyo ya kiserikali wala kisiasa, iliyoanzishwa kwa hiari kuleta maendeleo ya elimu.

Historia ya Elimu Miaka 1980–1992 skuli ya Kombeni ilikuwa maalumu. Mwaka 1997 wanafunzi 45 kidato cha pili, 4 tu wakajiunga kidato cha tatu (8%).

Skuli zilizolengwa

Bwefumu, Dimani, Kombeni Msingi/Sekondari, Maungani Msingi/Sekondari, Kisauni, Kitongani, Mombasa.

Changamoto: utoro (uvunaji kokoto, uvuvi, mkaa), mapenzi na starehe, mimba zisizotarajiwa, wizi wa mazao. Wazawa wameamua kuunda JUMEDI.

Dira · Dhamira · Imani

DIRA

Jumuiya imara, yenye kuwajibika – kuhamasisha, kunyanyua, kusaidia, kusimamia na kuelimisha jamii kwa maendeleo endelevu ya maisha bora ya wanafunzi.

DHAMIRA

Kuwajengea uwezo wanafunzi kuchangia kupunguza umaskini na kuimarisha utawala bora – kwa elimu bora ndani na nje ya Dimani.

THAMANI

JUMEDI yenye ubunifu, huduma kwa wote bila kubagu rangi, dini, jinsia wala itikadi za kisiasa.

Imani ya JUMEDI: Binaadamu wote ni sawa; kujituma halali kupunguza umaskini; elimu bora kuisaidia Serikali; Jumuiya kwa maendeleo ya wote – Dimani kiutawala.

Malengo 12 ya JUMEDI (Ibara 2.4)

  • Kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo ya elimu
  • Kukuza viwango vya elimu kwa vijana
  • Kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi za elimu
  • Kusimamia elimu chekechea, msingi, sekondari, watu wazima
  • Kuwaendeleza vijana walioshindwa mitihani – Vituo vya Amali
  • Kuwajengea uwezo na mazingira bora ya ajira
  • Kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo
  • Kupiga vita UKIMWI, madawa ya kulevya na adui ujinga
  • Kuanzisha miradi kusaidia kutekeleza malengo
  • Kufanya jambo lolote lenye maslahi kwa wanachama na wananchi
  • Kuelimisha jamii Sera za Elimu, Afya, Mazingira
  • Kuendeleza na kulinda silka, tamaduni na mila za watu wa Ndaambani

Muundo na Uongozi

Mkutano Mkuu

Hukutana mara moja mwaka; wanachama wote.

Baraza la Uongozi

Mwenyekiti, Makamo, Katibu, Naibu Katibu, Mshikafedha, Msaidizi, Wajumbe Maalumu 6, Viongozi wa Idara.

Bodi ya Wadhamini

Sifa za Mwenyekiti Mtanzania, umri 30+, kidato cha 6, aliyeishi Ndaambani miaka 10 (kama sio mzaliwa).

Katibu: Kuhifadhi kumbukumbu, kuandaa vikao, mawasiliano, ripoti.

Mshikafedha: Kuandaa bajeti, kuhifadhi fedha, malipo kwa idhini.

Wajumbe Maalumu (6): Kusimamia sera, bajeti, utawala na utekelezaji.

Uanachama, Haki, Ada na Wajibu

Sifa

  • Akili timamu, umri 18+
  • Anakubalika jamii
  • Anamiliki/hamiliki kitega uchumi
  • Fomu ya usajili

Ada

Kujiunga Tsh 2,000

Mwezi Tsh 500 · Mwaka Tsh 6,000 (zinaweza kubadilika)

Aina

Waanzilishi (wastahiki), Wanachama wa kawaida, Walioteuliwa na Baraza.

Haki 9 za mwanachama – kuchagua/kuchaguliwa, kuhudhuria, kukagua vitabu (kwa idhini), kushitaki, kujitetea, kuhoji n.k.
Wajibu: kushiriki, kulipa ada, kuilinda Jumuiya, kuhudhuria vikao.
Kuachishwa: hiari, kuvunja masharti, kutolipa ada mwaka+1, kifo, uamuzi wa Baraza.

Idara Ndogondogo (3)

Mipango, Fedha na Uchumi

Bajeti, kutafuta fedha na miradi, ripoti za fedha.

Taaluma na Utafiti

Elimu kwa wote, kutatua changamoto, utafiti wa kina.

Habari, Wanawake na Uhamasishaji

Uhamasishaji afya, UKIMWI, kujiajiri, kupambana na unyanyasaji.

Uchaguzi Huru na wa Haki

Kila baada ya miaka 3 viongozi huchaguliwa kwa kura za siri katika Mkutano Mkuu.

Kamati ya Uchaguzi: wajumbe 3-5, huundwa mwezi 1 kabla, Mwenyekiti wa Kamati ndiye msimamizi mkuu.

Namna ya kuendesha

  • Maelezo ya wagombea mbele ya mkutano
  • Kura ya siri – karatasi maalumu
  • Wakala mmoja kwa kila mgombea
  • Mshindi kura nyingi; zikiwa sawa – marudio

Hazina na Ukaguzi

Fedha zatokana na: ada, misada, miradi, harambee. Akaunti Benki ya Watu wa Zanzibar.

Fedha zinatunzwa na Mshikafedha, chini ya Kamati Tendaji na Bodi ya Wadhamini.

Ukaguzi: Mara moja kwa mwaka na mkaguzi wa nje (Serikalini). Taarifa huwasilishwa Mkutano Mkuu.

Mabadiliko ya Katiba & Mawasiliano

2/3 ya wajumbe wanahitajika kurekebisha Katiba (Mkutano Mkuu).

Makao Makuu: Shehia ya Kisauni, Wilaya Magharibi “B”, Unguja.
Barua: S.L.P 1576 Zanzibar · Email: jummedi@yahoo.com
Imesajiliwa chini ya Sheria ya Jumuiya Namba 6 ya 1995. Haina faida.